Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, November 1, 2010

Vincent Nyerere ashinda Ubunge Musoma MjiniVincent NyerereTaarifa hii inatoka kwenye blogu ya Madaraka Nyerere akisema kuwa,

Taarifa rasmi iliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi wa Musoma Mjini, saa 11:30 alfajiri hii, imethibitisha ushindi wa Vincent Nyerere wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa mbunge mpya baada ya kumshinda aliyekuwa mbunge, Vedasto Mathayo Manyinyi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Matokeo rasmi ni haya:

Vincent Nyerere (CHADEMA) -------------------------- 21,335 (56.71%)
Vedasto Mathayo Manyinyi (CCM) --------------------14,072 (39.38%)
Mustapha Juma Wandwi (Civic United Front) -----------253 (0.71%)
Chrisant Ndege Nyakitita (Democratic Party) -------------53 (0.15%)
Tabu Saidi Machibya (NCCR - Mageuzi)---------------------19 (0.05%


from: http://www.wavuti.com/habari.html#ixzz140EemPXE

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ALIVYOPIGA KURA KIJIJINI KWAKE KIBAONI!!Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipiga kura kwenye kituo cha uchaguzi kijijini kwake, Kibaoni, Katavi Oktoba 31, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

a href="http://2.bp.blogspot.com/_Xo6k8kXBJ3M/TM4-2iGjkeI/AAAAAAAAB_E/-JoNkGABnpc/s1600/p+026.jpg">
Mke wa Waziri Mkuu. MamaTunu Pinda akipiga kura kwenye ituo cha Uchaguzi kijijini Kibaoni, Katavi, Oktba 31, 2010. (Picha na Ofisi ya WAziri Mkuu)

Huduma ya Vodafone M-PESA yaongoza kimataifa

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imetajwa kuwa ni kampuni bora kwa utumaji wa fedha ulimwenguni kupitia huduma yake ya Vodafone M-Pesa.
Taarifa hiyo ilitolewa ilitolewa wakati wa maonyesho ya kwanza yanaohusu huduma za utumaji pesa kwa njia ya simu za mkononi yaliyofanyika Dubai tarehe 25 mwezi huu.Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare alisema taarifa hiyo iliyopatikana wakati wa maonyesho hayo imeipa faraja kampuni yake .“Taarifa hiyo inatambua mchango na viwango vya huduma zetu kwa wateja pia , alisema Mkurugenzi hiyo

Bw. Mare alisema kwamba Kampuni hiyo haitabweteka kwa sababu imepata heshima hiyo kubwa Ulimwenguni kwa wa watoaji kwa huduma na bidhaa bora na badala yake itaboresha huduma zake.Hivi karibuni kampuni hiyo ilishinda tunzo ya Chapa Bora kwa Afrika Mashariki , ili kushinda tunzo hiyo vigezo mbalimbali huzingatiwa ikiwamo unora wa bidhaa.Bw. Mare aliwashukuru wateja wote wa Vodacom kwa uaminifu wao na kuwahakikishia kwamba wataendelea kuwapatia huduma bora wateja wake ili waweze kukata kiu yao ya mawasiliano na sanjari na huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo.“Tutaendelea kuwapatia wateja wetu huduma bora ambazo zitakidhi kiu yao ya mwasiliano lakini katika hali ambayo wataimudu na yenye manufaa kwao,”Vodafone M-PESA, ni njia rahisi ya utumaji pesa kwa njia ya simu za mkononi, njia hi ilizinduliwa rasmi mwaka 2008, kwa hapa nchini huduma hiyo imekubalika na inatumiwa na Watanzania wengi.


Wateja wa Vodafone-MPESA sasa wanaweza kulipia huduma mbalimbali kama vile LUKU, bili za Dawasco, kuongeza muda wa maongezi, kutuma na kupokea fedha kwenda mtandao wowote hapa nchini na kulipa ada za wanafunzi.Hadi sasa huduma hiyo ina wateja zaidi ya milioni 5.4 waliojisajili sajiliwa katika huduma, huku kila mwezi wateja wapya 500,000 wakisajiliwa.Hivi sasa zaidi ya shilingi bilioni mia sita 600 zimeshatumwa kupitia mtandao huo huku idadi ya mawakala ikiwa ni 5000 nchini kote

BRAZIL ELECTS ITS FIRST WOMEN PRESIDENT!


Ms Rousseff had 55.8% of the votes against 44.2% for centrist candidate Serra with more than 97% of the total counted.

She will be sworn in as President on January 1 next year.

Ms Rousseff, 62, a career civil servant who has never held an elected office before, was bolstered by the support of President Luiz Inacio Lula da Silva.

As polls opened, Ms Rousseff paid tribute to Mr Lula, and assured Brazilians that while he would not have an official role in her government, he would always be near.

"President Lula, obviously, won't be a presence within my cabinet," she said at a final campaign stop in her hometown of Belo Horizonte.

"But I will always talk with the president and I will have a very close and strong relationship with him.

"Nobody in this country will separate me from President Lula."

Ms Rousseff pledged to continue Mr Lula's popular social programmes which have helped take 20 million Brazilians out of poverty since he took office in 2003.

With about 135 million voters, Brazil's powerful economy has helped it achieve an important position as a key emerging nation.

Latin America's largest country is also a world leader in bio-fuel development, while simultaneously working to develop massive deepwater oil fields.

Ms Rousseff will lead a nation due to host the 2014 World Cup and the 2016 Summer Olympics, by which time it is expected to be the globe's fifth-largest economy.

"I want to unite Brazil around a project not just of material development, but also of values," she said.

"When we win an election, we must govern for all Brazilians without exception."

Mr Serra, 68, is a former governor of Sao Paulo state and one-time national health minister who was heavily defeated by Mr Lula in the 2002 presidential election.


For more news visit: www.skynews.com

Wednesday, October 20, 2010

Zitto anadi gwanda, achangisha 800,000/- papo hapo!Kampeni za Naibu Katika Mkuu wa CHADEMA Taifa, Zitto kabwe, katika jimbo la Sumbawanga mjini zimeendelea kuiweka pabaya CCM kutokana na kampeni zake kuwachambua kinagaubaga.
Watu zaidi ya 2,000 walifanya maandamano ya furaha kwa kumsindikiza mgombea ubunge wa jimbo hilo Mwalimu Norbert Yasembo. Pia, walitumia mkutano wa kampeni za CHADEMA kumchangia mgombea huyo fedha za kuwalipa mawakala wake kiasi cha shilingi zaidi ya 800,000/- katika harambee iliyoendeshwa na Zitto ambaye pia alijitolea kuchangia kampeni hizo kwa kuuza kombati yake kiasi cha shilingi 200,000/

Akihutubia katika mwendelezo wa mikutano ya kampeni ya CHADEMA mkoani Rukwa katika viwanja vya Rukwa High School jana, mbali ya kukataa kata kata dua za wananchi hao kumwombea kuwa Spika wa bunge lijalo la Muungano wa Tanzania, Kabwe alisema kuwa lazima CCM itambue kuwa hatua ya wananchi kuchangia kiasi hicho cha fedha ni mwisho mbaya kwake na kuwa itegemee kushinda kwa miujiza jimbo hilo.

“Nasema napongeza sana kwa mapokezi haya makubwa ambayo mmeonyesha kwangu na huu ni ushadidi kuwa mgombea wa CCM katika jimbo hili Aesha Hillary si chaguo halisi la wana jimbo la Sumbawanga mjini hivyo si vizuri kwa wachache waliobaki kupoteza kura zao kwa kumpa mgombea ambaye hatakiwi “

Alisema kuwa mkoa wa Rukwa, Kigoma na Tabora ni mikoa ambayo makao makuu yake bado hadi sasa hajaunganisha na lami hali ambayo inahitaji kuwapata wabungemakini watakaoweza kutetea wananchi wa mikoa hiyo kuwa ni sehemu ya wananchi wa mikoa ya Tanzania ambayo kwa sasa imeunganishwa kwa lami .

“Ndugu zangu, Tanzania ni moja na mikoa yote ya Tanzania wananchi wake ni walipaji wakubwa wa kodi, hivyo kitendo cha Serikali ya CCM kuendelea kuwabagua wananchi wa mikoa hiyo ni sawa na kuwaona kuwa hawafai kupewa huduma hiyo na dawa pekee ni wananchi wa mikoa hiyo kuunga na kuwanyima kura wagombea ubunge wa CCM na kuwapa wale wa CHADEMA ambao kupitia Rais mpya wa awamu ya tano kwa Tanzania Dk Wilbrod Slaa, wananchi wa mikoa hiyo wanapewa haki yao ya lami”

Kabwe alisema kuwa wananchi wa Tabora, Kigoma na Rukwa wasipokubali kuunganisha nguvu zao katika kuchagua wabunge wa CHADEMA, bado CCM itaendelea kuwafanya kuonekana kuwa wanyonge. Aliongeza kuwa, katika mkoa wa Kigoma kwa bunge lililopita mbunge wa upinzani alikuwa ni mmoja pekee huku katika mkoa wa Rukwa pia kulikuwa na mbunge moja hivyo ni vizuri Oktoba 31 wakaongeza idadi zaidi ili kuwe na idadi kubwa ya wabunge.

Hata hivyo, alisema kuwa kwa upande wake hana tatizo la jimboni kwake kwani tayari ameshinda na anasubiri kuapishwa na Rais wake Dk Slaa.

Katika hatua nyingine, Kabwe ameshangawa na hatua ya ulinzi mkali aliowekewa katika jimbo hilo la Sumbawanga mjini ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha askari polisi, askari magereza, pamoja na mgambo kufika kulinda mkutano jambo ambalo hajapata kuona askari magereza wakifika katika mikutano ya kampeni kama jimbo hilo la Sumbawanga mjini na kuwa yawezekana katika mkutano wake huo, wafungwa pia wamefunguliwa ili kujakusikiliza sera za CHADEMA.

Katika mkutano huo uliomalizaka kabla ya muda wa kampeni kuisha, wananchi walifanya maandamano makubwa huku biashara zao zikisimama kwa muda kwa ajili ya kusukuma gari la Zitto Kabwe pamoja na ile ya mgombea ubunge wa CHADEMA huku wakiimba kuwa wanataka mbunge Msomi wa CHADEMA sio CCM. Hatua hiyo ilionyesha kuwapa wakati mgumu askari polisi magereza na wale wa jeshi la polisi nchini kuwatuliza wananchi hao na kuwaomba viongozi wa CHADEMA kuwatuliza na kuwatawanya wananchi hao zaidi ya 2,000 kabla ya mgombea ubunge wa CHADEMA kuamua kuwatoroka viongozi wenzake ofisini ili waandamanaji hao watawanyike.

from: http://www.wavuti.com/4/post/2010/10/zitto-anadi-gwanda-mkutanoni-achangisha-800000-papo.html#ixzz12sZxXuaZ

MWANAFUNZI CHUO AVUTA MSHIKO WA SUPERHuku droo ya Supa Pesa ikiendelea kutoa mamilioni kwa washindi wake kupitia bahati nasibu inayochezeshwa nchini kote, wikiendi iliyopita imemkuta mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dodoma,tawi la Mwanza, Catherine Nyamoni, akibahatika kujinyakulia kiasi cha milioni moja fedha taslimu.Mwanafunzi huyo, mwenye umri wa miaka 23, alisema,’ Kweli mimi nilikuwa kati ya watu ambao sitilii maanani michezo ya bahati nasibu wala kuwahi kushiriki kati shindano lolote maishani mwangu. Lakini wiki chache zilizopita nilipokuwa nasikiliza redio nyumbani, nilipata nafasi ya kumsikiliza mshindi wa milioni kumi akipigiwa simu kujulishwa kuhusu ushindi wake.
Basi pale ndipo nilipata hamasa kubwa na kuamua kutopitwa na nafasi ya kujaribu bahati yangu. Nilishiriki kwa kutuma ujumbe mfupi kama walivyoelekeza na baada ya kujaribu mara kadhaa nimepata ushindi. Namshukuru Mungu nimefanikiwa na kupata ushindi.’Catherine aliongezea kusema, ‘ Nitatumia hela za ushindi kuendeleza masomo yangu kwa kununua kompyuta itakayonisaidia kufanya kazi chuoni kwa ustadi zaidi na vilevile hela itakayobaki ninatarajia kutumia kama mtaji wa kuanzisha biashara ndogo ili kujipatia kipato cha kila siku.Kushiriki droo ya Supa Pesa ni rahisi, inahitaji kutuma ujumbe mfupi wenye neno SUPA kwenda namba 15777. Hii inakuwezesha wewe kuingia moja kwa moja kwenye ushindani wa shilingi milioni moja kila sikui na ukishiriki kutuma Ujumbe mfupi wa simu zaidi ya mara nne basi utakuwa kati ya washindani wa milioni kumi kila wiki.

Tuesday, October 12, 2010

JK Akiwa Mbinga1. Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)
Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mtoto mlemavu Maria Chiwinga muda
mfupi baada ya kuwasili mjini Mbinga jana ambapo aliwahutubia wananchi
katika mkutano mkubwa wa kampeni.Dr.Kikwete aliahidi kumpatia mlemavu
huyo msaada ili aweze kuendelea vyema na masomo yake.

2.Wananchi wa mji wa Mbinga wakimkaribisha kwa ngoma mgombea
urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili mjini
hapo na kufanya mkutano mkubwa wa kampeni.

3. Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi mgombea ubunge jimbo
la Peramiho Jenister Mhagama wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika
katika kata mpya ya Mtyangimbole, jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma jana